SIPHO Makhabane si jina geni katika tasnia ya muziki wa injili
barani Afrika.
ukifananisha na majina ya wanamuziki wengine kama Joyous
Celebration ama Sfiso Ncwane, Rebecca Malope yeye ni mmoja wa magwiji wa
uimbaji nchini kwake Afrika ya kusini akiwa ameshiriki katika shughuli
mbalimbali za kiroho na kijamii.
Makabane mwenye umri wa miaka 45 amekuwa akisifika na kuvutia
mashabiki wake kwa mtindo wa nyimbo zake na uchezaji.
Gwiji huyo wa muziki wa injili alitangaza kustaafu uimbaji mnamo
mwaka 2010 ingawa mwaka jana alitoa albamu nyingine mpya akiwa ana miliki
kampuni kubwa inayotoa wanamuziki wapya kila kukicha ya "Big Fish".
Historia yake inaeleza kuwa aliacha shule akiwa darasa la tano
kutokana na ugumu wa maisha na kuamua kufanya kazi katika shamba la miwa la
Kaaruls huko Mpumalanga ili aweze kuwasaidia ndugu zake na mama yake ambao
walikuwa wakimtegemea yeye.
Makabane alipotimiza miaka 17 alihamia kwenye kazi za ujenzi
kwenye mbuga ya ‘Kruger National Park’ ambako alishiriki katika ujenzi wa
nyumba kambini hapo.
Akiwa na miaka 21 alikuwa tayari na ujuzi wa kutosha katika kazi
ya ujenzi ambapo alipata kazi Pienaar kabla kupata ofa nzuri katika kampuni ya
Telkom mnamo mwaka 1986 kama fundi, huku muda wote huo akipenda sana muziki wa
injili lakini pia ndio ulikuwa mwanzo wake katika biashara na kujua kwamba
atatengeneza pesa nyingi kupitia uimbaji.
Akiwa na miaka 25 alifunga ndoa na mkewe ambaye kwa wakati huo
alikuwa na miaka 18 hiyo ilikuwa mwaka 1990 na kuanza shughuli ya kununua na
kuuza kazi za muziki ndani na nje ya nchi yake.
Lakini kwa wakati huo akifanya kazi katika kampuni ya Telkom
hamu ya moyo wake ilikuwa ni kurekodi albamu yake binafsi na kufanikiwa kufanya
hivyo na kuonyesha kabisa kupenda kazi ya uimbaji kuliko kuweka sawa mitambo ya
simu,lakini ilikuwa shida kuwavutia wasambazaji ambao alitaka wawe wananunua
kazi kutoka kwake huku wakiwa hawaamini kama ana uwezo huo wa uimbaji mpaka
pale waliposikia kazi yake katika moja ya radio maarufu nchini humo ya Swazi
a.k.a Ligwalagwala FM.
Mkabane alitambulishwa na wimbo wa 'Ngitinikela Kuwe' ambao ndio
ulikuwa wa kwanza na mwaka 1996 gwiji huyo akaamua kujikita kwenye tasnia hiyo ya
muziki wa injili na kuachana na kazi yake kwenye kampuni ya simu.
Mwaka 1996 aliachia albamu iitwayo ‘yek'intokozo’ wimbo ambao
mpaka leo umeacha alama kwa mashabiki wake kwa kumtambua vyema kupitia wimbo
huo.
Lakini wakati huo tayari alishatoa albamu nyingine mbili miaka
ya 1993 hadi 1999 zikiitwa "THUM'UMLOLO" na "JESU
ULIQHAWE".
Mwaka 1998 kupitia kampuni ya CCP Records aliachia albamu yake
ya nne iitwayo "Uyigugu" iliyofanya vyema, mwaka 1999 akaachia album
iitwayo "Makadunyiswe" moja ya album ambayo inapendwa sana na
mashabiki.
Mwaka 2001 akaachia albamu ya Calvary ambayo iliuza kufikia
kiwango cha unit 21.
Mwaka 2002 akaachia ''Akukhalwa"iliyokuwa kama albamu yake
ya "Yek'intokozo" ambapo iliuza zaidi ya nakala 70,000, mwaka 2003
akaachia albamu ya ''Moya wami" ambayo pia iliuza zaidi ya nakala 70,000.
Sipho Makhbane ameshirikiana katika albamu na waimbaji wakongwe
wa nchini kwake kama Jabu Hlongwane, Marehemu Vuyo Mokoena, Lundi, Hlengiwe
Mhlaba na wengine wengi pia akiwa nyuma ya mafanikio ya waimbaji lukuki kama
Hlengiwe Mhlaba, Ncandweni Christ Ambassadors, Shongwe na Khuphuka Saved Group,
na pia akiwa mtayarishaji wa albamu za waimbaji wengi.
Mwaka 2004 aliachia albamu ya "Nkosi nghibheke" ambayo
ilikuwa na vigumu kwa mashabiki wake kuchagua nyimbo zilizomo kwakuwa zote
zilikuwa nzuri huku kibao cha "guyizolo" ambacho kilikuwa cha
shukrani kwa Mungu ambaye huwa anamtumaini kwa kila kitu, pia aliamua kutoa
albamu ya muziki tupu au ala kupitia albamu hiyo.
Mwaka 2005 aliachia albamu chini ya kampuni ya SONY/BMG iitwayo
"Umuzi Omuhle" akimshirikisha mwanamama Hlengiwe Mhlaba
ikimtambulisha kimataifa zaidi, kama haikutosha aliachia album yake ya 15
''Ngiyamemeza" ikiwa ni albamu yake ya tatu kutoa chini ya SONY/BMG bila
kusahau nyimbo alizokuwa akizitoa kila wakati wa pasaka na kubariki watu wengi
huku kampuni yake ikiwa ni moja ya kampuni kubwa kabisa nchini Afrika ya
kusini.
Amewahi kuimba jukwaa moja na waimbaji kama Kirk Franklin
akipata tuzo mbalimbali kama SAMA, Crown, na nyinginezo ikiwemo kutajwa kwenye
tuzo za Kora ambazo zilikuwa maarufu barani Afrika.